Tasfida Katika Bunge

Maana ya tasfida

Tasfida ni kutumia maneno mazuri, matamu yanayopendeza, yaliyotiwa nakshi yakavutia. Pia ni kutosema maneno moja kwa moja ili kuepuka kudhuru uso wa msikilizaji.

Tasfida ni ile hali ya kutoa maana hasi na kutia maneno urembo na nakshi ili yaonekane kuwa mazuri.

TUKI inasema kwamba tasfida au usafidi ni matumizi ya maneno ya staha badala ya yale halisi. Kwa mfano, aga dunia ni neno la staha na lenye upole linalotumika badala ya neno kufa.

Tasfida huruhusu wanajamii kuzungumza vitu visivyofaa kwa njia ifaayo ili kuvipunguza makali.

Kamusi ya Karne ya Ishirini na Moja (2011) inatafsiri tasfida kama tamathali ya usemi inayotumia lugha fiche badala ya kutumia lugha ya karaha au matusi.

Tasfida hutokana na maneno ambayo ni mwiko katika jamii.

Wamitila anasema kuwa tasfida ni mbinu inayotumiwa katika maongezi au lugha ya kila siku kufichia ubaya, uozo au uovu fulani kwa kutumia maneno au lugha ambayo inapunguza makali au uozo, ubaya au uovu unaozungumziwa.

Mifano ya tasfida

Katika Jarida la The Table, mbunge fulani alinukuliwa kule Bunge la Australia kusema “the snake charmer over there”. Mwingine akanukuliwa kusema, “What a hypocrite the Shadow Treasurer is, Mr. Speaker! What a pathetic hypocrite!”

Katika sajili ya bunge, matamshi yasiyo ya kibunge (unparliamentary language) ina maana ya kutumia maneno ambayo, kwa maoni ya kiongozi wa kikao, yanaashriria ujeuri, kukosa adabu, matusi au kutozingatia utataribu au desturi za Bunge.

Imetajwa katika Kanuni za Kudumu za Bunge (Standing Orders) kuwa ni utovu mkubwa wa nidhamu mbunge akikataa kufafanua au kuondoa maneno yasiyo ya kibunge au kukataa kuomba radhi licha ya Spika kumtaka kufanya hivyo.

Tazama mazungumzo

Ikiwa ungetaka kutazama mazungumzo haya kwa ukamilifu, hii hapa chini:

Asante sana ndugu Dan Mugera na Taasisi ya Ulumbi Afrika (The African Centre for Public Speaking) kwa kunialika katika jukwaa hili. Nitakuwa mchache wa fadhila nisipokupongeza kwa juhudi zako kwa hali na mali ya kufanikisha #nasahazauongozi. Wasemao husema aliyekalia kigoda mtii na asiyeweza kutuumba kutuumbua hawezi.

Mwenyezi Mungu aweze kukuneemesha, kiongozi.

_

ayes & nays

Spread the love